Thursday, October 3, 2013

NDEGE ILIOKUWA IMEWABEBA WATU 20 YAANGUKA UKO NIGERIA.

Ndege iliyokuwa imewabeba watu 20 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos.

Duru zinasema kuwa watu 8 wamefariki.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 30 ilianguka na kulipuka.

Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani nchini humo.

Injini ya ndege ilikumbwa na hitilafu na kuisababisha ndege kuanguka na kuteketea.

Hata hivyo hakuna taarifa za kuthibitisha idadi ya watu waliofariki.

  *********************

Mtandao mmoja wa Nigeria umeandika hivi

 An Associated Airline plane carrying 20 persons to Akure Ondo State  for the burial of former Ondo State governor, Olusegun Agagu  crashed  in Lagos airport fuel dump area minutes after take-off
Silverbird Tv reports that Spokes Person of the National Emergency Management Agency NEMA in the south west, Ibrahim Farinloye confirmed the incident said 8 bodies have been recovered from the site of the crash, 1 injured is being taken to the Lagos State University Teaching Hospital LASUTH
Unconfirmed Reports claim the plane was also conveying the only son of the late gov, his wife and the late Gov.corpse whose burial was set for tomorrow Friday 4th October 2013.
 


No comments:

Post a Comment