Waziri mkuu wa Libya ametekwa nyara na watu wasiojulikana na ambao walikuwa wamejihami kutoka nyumbani kwake mjini Tripoli.
Habari zinasema kuwa bwana Ali Zeidan (Pichani) ametekwa
nyara na kupelekwa katika eneo lisilojukana , lakini hakuna taarifa
zaidi kuhusu tukio hilo.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa huenda Zeidan amezuiliwa.
Mnamo siku ya Jumanne waziri mkuu Zeidan alitoa
wito kwa Marekani na nchi za Magharibi kukomesha vitendo vya wapiganaji
wenye itikadi kali nchini Libya.
Waziri huyo aliwai kunukuliwa, akisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.
Waziri mkuu huyo akaenda mbali na kudai kuwa nchi yake inatumika kama sehemu ya kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya kanda hiyo.
|
No comments:
Post a Comment