Wanasayansi wa nchini Uswizi wametoa lipoti yao ya uchuguzi wa kifo cha aliyekuwa kiongozi wa wapalestina Yasser Arafat Pichani na kubaini kuwa kiongozi huyo alipewa Sumu aina ya POLINIUM. Hata hivyo ripoti za awali kulingana na rekodi za kimatatibu zake
hayati Arafat zinasema kuwa alifariki kutokana na kiharusi ,
kilichosababishwa na ugonjwa wa damu.Lakini mwili wake ulifukuliwa mwaka jana kwa uchunguzi zaidi kutokana na madai kuwa Arafat aliuawa.Ripoti hiyo ya wanasayansi kutoka Uswizi,
inasema kuwa mwili wa Arafat ulionyesha dalili za kuwa na kiwango
kikubwa cha sumu ya Polonium, na hivyo kuunga mkono dhana ya kuuawa
kwake kwa sumu.Wapelestina wengi wameamini kwa miaka mingi kuwa
Israel ndio ilimuua Aarafat kwa sumu. Wengine wanadai kuwa alifariki
kutokana na ugonjwa wa Ukimwi au Saratani.Israel imekuwa ikikana madai ya kuhusika na mauaji ya hayati Arafat.Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Israel,
amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na wanasayansi wa Uswizi ni kama
mchezo wa kuigiza tu.Wanasayansi hao walifanyia uchunguzi wa kina
nyaraka za kimatibabu za Arafat, wakachunguza mabakai yake pamoja na
vitu alivyokwenda navyo hospitalini mjini Paris kutafuta matibabu
alipofariki mwaka 2004.Walifanyia uchunguzi mifupa yake pamoja na mchanga katika sehemu alikozikwa Arafat.Wanasayansi hao walisema kuwa matokeo ya utafiti wao yanawiana na madai ya Arafat kuuawa kwa sumu aina ya Polonium-210.
|
No comments:
Post a Comment