Sunday, September 14, 2014

PAMOJA NA KUAMIA AZAM ASHUHUDIA IKIPIGWA 3 NA TIMU YAKE YA ZAMANI YANGA.

Shabiki aliejipatia umaarufu mkubwa baada ya kuwa anaipenda Yanga kupitiliza hadi kupelekea mara kwa mara kutoa machozi pale ambapo anaona Yanga imeonewa au imefungwa sasa shabiki huyo anaejulikana kama Steve katika mchezo wa ngao ya jamii kati ya Azam na Yanga ameonekana akiwa amevalia jezi ya Azam akiishangilia kwa nguvu zake zote huku akishuhudia ikipewa kipigo cha paka mwizi cha mabao 3-0 katika mchezo huo.Picha hapo chini wakati akiwa shabiki wa Yanga.

Hapa akimpokea Okwi wakati alipowasili baada ya kusajiliwa Yanga.



Sunday, June 15, 2014

Word Cup:Balotelli apeleka kilio wingereza ,Ivory Coast nayo yachanua

Michuano ya Kombe la Dunia inaendelea uko Brazil katika michezo iliopigwa jana na kuamkia alfajili ya leo Jumapili kwa masaa ya Afrika mashariki Matokeo ni kama ifuatavyo.

ITALY 2 ENGLAND 1

IVORY COAST 2 JAPAN 1



Friday, June 13, 2014

HII SI BRAZIL BALI NI USAILI WA UHAMIAJI UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM.

Kwa haraka haraka unaweza kusema kuna Mpira unaendelea Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam hivi sasa kumbe sio mpira bali ni katika harakati za kutafuta ajira na leo ndo siku ya Usaili kwa wale walioomba Uhamiaji hapa ndipo utajua kweli WATU KUTOPATA AJIRA NI JANGA LA KITAIFA SERIKALI INABIDI KULITAFUTIA UFUMBUZI WA HARAKA NA MAPEMA SANA.

Wakisubili kuitwa katika usahili huo.
Wakiingia ndani ya uwanja tayari kusubili usaili.

UFUNGUZI KOMBE LA DUNIA ULIVYOKUWA (PICHA)


Friday, May 23, 2014

BAADA YA KUDAIWA KUFANYA FUJO BAR HIVI NDIVYO MAGAZETI YALIVYOMUANDIKA MOYES.

Baada ya kudaiwa kumshambulia mtu Bar na Polisi kulipotiwa kuanza kuchuguza tukio hilo linalodaiwa kufanywa na  Kocha wa zamani wa Machester United David Moyes hivi ndivyo magazeti ya wingereza yalivyoandika khusu tukio hilo.

Monday, May 19, 2014

Hatimaye Machester United yatangaza Rasmi Kocha wake kwa msimu ujao.

Louis Van Gaal ndio Kocha Mpya wa Klabu ya Machester United anachukuwa nafasi iliokuwa wazi baada ya kutimuliwa kwa Kocha David Moyes. Klabu ya Machester kwenye taarifa yake imesema kocha huyo mpya atasaidiwa na Ryan Giggs kama kocha msaidizi.

Louis Van Gaal muholazi aliefundisha klabu mbalimbali kama  Ajax Amsterdam mwaka 1995,akiwa na klabu iyo aliweza kushinda kombe la Mabigwa Ulaya,Mwaka 1998 na 1999 alishinda la liga ligi ya Hispania akiwa na klabu ya Barcelona na Badae akiwa na klabu ya Bayern Munich nae aliweza kutwaa taji mwaka 2010.



Sunday, May 4, 2014

DIAMOND KAVUNJA REKODI YA TUZO ZA KILI MUSIC ACHUKUA TUZO 7

Hatimaye zile Tuzo za Muziki Tanzania Zinazojulikana kama Kili Music Award ndio zimemalizika na Mwanamziki Diamond Kuibuka na Tuzo saba katika Vipengele tofauti tofauti.

 


Monday, April 14, 2014

HATIMAYE HATI HALISI YA MUUNGANO ITAWASILISHWA BUNGENI SIKU MBILI ZIJAZO.

Mwenyekiti wa kamati namba Sita Mh.Stephen Wasira kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amethibisha rasmi leo ndani ya Bunge la Katiba na kwa wananchi wa Tanzania kuwa Hati alisi ya Muungano ilisainiwa na Marais wawili Mwl.Julius Nyerere na Mwezake Abed Karume miaka hamsini iliopita ipo na itwasilishwa rasmi katika Bunge la Katiba ndani ya siku mbili zijazo,namnukuu Wassira: Nalihakikishia Bunge kuwa Hati ya Muungano wa Tanzania ipo na itawasilishwa Bungeni siku mbili zijazo!

Kwa hatua hiyo ya kuitoa Hati halisi ya Muungano itakuwa imesaidia kupunguza maneno kutoka Baadhi ya wajumbe kuwa hati hiyo aipo na kama ipo basi si halisi bali itakuwa imechakachuliwa.

Wakati mijadala ya kamati ikiwa inaendelea kuliibuka swala la wajumbe kutaka wapatiwe hati ya muungano na hata ilipopatikana ilionekana kama baadhi ya saini zilizopo zimegushiwa.

 Leo aliekuwa Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya muungano mzee Pius Msekwa alipokuwa amazungumza kupitia kituo cha tv cha Taifa (TBC1) Amesema kuwa kuwa hakuwahi kuziona na wala hazikuwahi kuletwa bungeni badala yake, kile kilicholetwa bungeni ile tarehe 25/04/1964, ili kuridhia hati hizo, sio Hati Halisi za Muungano, bali ililetwa Sheria ya Muungano, ikiwa imeambatanishwa na "a schedule" ya Hati Hizo, iliyokuwa imepigwa chapa tuu, bila saini yoyote!.

 


Sunday, April 13, 2014

LIVEPOOL 3 MANCITY 2 .

Mpira umemalizika kati ya Liverpool na Manchester City na liverpool kuibuka na ushidi wa Mabao 3 kwa 2.Liverpool walikuwa mbele kwa mabao 2 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika kwa magoli ya Halftime na Skirtel dakika ya 26.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana na kupelekea Man City kurudisha magoli hayo yaliofungwa na Silva dakika ya 56 pamoja na Johnson aliejifunga kwenye Dakika ya 63 Goli la ushidi la liverpool limefungwa na beki wa Machester city na naodha wa Timu hiyo Vicent kwa matokeo hayo Liverpool imezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu wingereza kwa point 77


GWIJI WA MZIKI WA DANSI MUHIDIN GURUMO ATUNAE TENA KATIKA DUNIA HII.

Mwanamziki na Gwiji wa mzuziki wa dansi nchini Tanzania mzee Muhidin malimu Gurumo alikuwa kiongozi wa Bendi ya Msondo ngoma  amefariki majila ya mchana katika Hospitali moja alipokuwa akipatiwa matibabu.


Habari za hivi punde:Elkopta ya Polisi imeaguka Dar es salaam.

Habari za awali zinasema kwamba kulikuwa na baadhi ya viongozi waliokuwa katika ziara ya kukagua athali za mafuriko jijini Dar es salaam

Habari zinazoendelea kupatikana ni kwamba ilikuwa na Kamanda wa Polisi wa kanda maalum pamoja na Mkuu wa mkoa lakini wanaendelea vizuri habari zaidi zinafuata......... 

 Habari zaidi zinasema pia kulikuwa na makamu wa rais katika msafara huo



MANNY PACQUIAO AMSHIDA TIM BRADLEY

Pambano la ngumi kati ya Manny Pacquiao na Tim Bradley limemalizika mda mfupi uliopita kwa Manny kushinda kwa point kama ambavyo Bradley alivyoshinda kwenye pambano la kwanza kati yao ingawaje baadhi ya watu hawajalidhika na ushidi huo na kusema ni kama alioupata Tim katika pambano la kwanza wa utata utata.

 


Saturday, April 12, 2014

ARSENAL HATIMAYE WATINGA FAINALI YA KOMBE LA FA.

Hatimaye Timu ya Arsenal sasa imejiweka katika mazingila mzauri ya kuibuka na kikombe msimu huu baada ya kutiga Fainali ya chama cha mpira cha wingereza maarufu kama Kombe la FA baada ya kuifunga timu ya wigani kwa Penati 4 kwa 2 za Wigan baada ya kumaliza mchezo huo kwa kufungana magoli 1 kwa 1

  Kipa wa Arsenal akiokoa moja ya Penati



HII IMETOKEA LONDON MAMA MMOJA AMFANYA MBWA MWANAUME MMOJA.

Unaweza ukadhani ni mchezo wa kuigiza lakini kumbe ni kitu ambacho ni kweli kimetokea katika mtaa mmoja mjini London ambapo Mama mmoja mida ya asubuhi alipoonekana akielekea katika shughuli zake huku akiwa ameambatana na Mwanaume lakini mwanaume huyo akiwa amefungwa kamba mithili ya Mbwa kama unavyojionea katika Picha

 Baadhi ya watu walionekana kushangazwa na tukio hilo ambapo mmoja wao alieshuhudia alisema namnukuu katika lugha ya Kingereza "Officially say weirdest thing.. Woman walking a man to work.. On a lead... On his hands and knees... Seriously!?!?". 

 Huko Nyumbani East Afrika wanaume mnasemaje juu ya tukio hili kama huko nako yanatokea tutumie katika anuani yetu hapo juu utuambie pamoja na mtazamo wako unafikilia nini kwa nini Mama huyu kafanya hivyo.


Thursday, April 3, 2014

PICHA YA SIKU NA NI PICHA YA KIHISTORIA.

Kila mwishoni mwa wiki kupitia Blog hii huwa tunawaletea Picha zinazokuwa na mvuto katika Nchi mbalimbali Duniani katika mitandao ya kijamii na kwenye Magazeti katika nchi husika leo Picha iliochukua nafasi ni picha hii inayomuonyesha POPE FRACIS AKIWA NA MALKIA WA WINGEREZA .


Saturday, March 29, 2014

MCHEZAJI WA ARSENAL ALICHOPOST KUHUSU TANZANIA PAMOJA NA PICHA.

Baada ya Mchezaji wa Arsenal Lucas Podolski kuiona picha hii hapo chini jamaa akiwa amevaa jezi namba 9 ya timu yake anayochezea ndio ikampelekea kuandika tweet hiyo hapo juu.

 


Thursday, March 27, 2014

RAIS BARACK OBAMA KWA MARA YA KWANZA AKUTANA NA POPE.

Hatimaye kwa mara ya kwanza Rais wa Marekani Barack Obama amekutana na Baba mtakatifu Pope Francis mjini Vatican katika ziara hiyo ya Obama inategemewa mambo yatakayo zungumzwa pamoja na kiongozi huyo wa kiroho wa Madhehebu ya kikatoliki Duniani yenye waumini wengi Duniani ni pamoja na swala la swala la Ushoga na Umasikini.

 


"KUNA NJAMA ZA KUVURUGA BUNGE LA KATIBA" - SITTA

Baada ya jana jioni kuahirisha Bunge hilo baada ya kutokea sitofahamu ya kubadilisha kanuni, Sitta alikutana na waandishi wa habari na kusema kwamba kuna njama za baadhi ya wanasiasa kutumia vurugu kuhujumu mchakato wa upatikanaji wa Katiba, badala ya kujenga hoja.

Bila kuwataja wanasiasa hao, Sitta alisema ikiwa hawataki kuendelea na mchakato huo, basi waondoke na kuwaacha wenye nia njema.

“Wanasiasa hawa wamedhamiria kuvuruga mchakato wa Katiba, tuhuma ambazo tumetuhumiwa leo na Lissu (Tundu) ni uongo na uzushi, mimi sihusiki na kupeleka marekebisho ya kanuni kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge,” alisema Sitta.

Sitta alikuwa anajibu mchango wa mjumbe wa Bunge, Tundu Lissu alioutoa mapema kwenye kikao cha jioni, akipinga kilichoelezwa ni njama za kutaka kubadili kanuni kinyemela ili kumsaidia mwenyekiti kulidhibiti Bunge.

Sitta alisema kwa kuzingatia kanuni ya 59 (1), Kamati ya Uongozi ina mamlaka ya kupeleka marekebisho ya kanuni ili kuliwezesha Bunge kufanya kazi vizuri.

Alisema hoja kwamba haiwezekani kufanyika mabadiliko hata kabla ya kuanza kutumika kanuni, siyo ya msingi kwani kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira yake.

“Kamati ya Uongozi ndiyo ilipeleka waraka wa mabadiliko ya kanuni kwa Kamati ya Kanuni na Haki kwa kuzingatia kanuni, lakini hata kabla ya kujadiliwa na kamati husika inaonekana kuna wajumbe ndiyo wameichukua na kuifikisha bungeni,” alisema Sitta.

Alisema kwa kiasi kikubwa marekebisho ambayo yangesomwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pandu Ameir Kificho, yalilenga kutoa ufumbuzi wa kanuni ya 37 na 38 juu ya upigaji kura ama uwe wa wazi au siri.

Sitta alisema pamoja na hilo, kulikuwa na marekebisho ya msingi kama kuweka utaratibu mzuri wa majadiliano katika kamati pia kuweka utaratibu wa vikao vya Bunge kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.

“Mengi ambayo alikuwa anayasema Lissu kama ni takataka hayakuwapo katika taarifa ya Kificho,” alisema Sitta.


Wednesday, March 26, 2014

KIM KARDASHIAN SAFARI HII NA ILI VAZI!!!!!

Mwana Mama Kim Kardashian mwenye miaka 33 akiwa na mtoto mmoja aliempata kutoka kwa rapa Kanye west siku ya Jumatano alitokelezea kwenye kipindi kimoja cha talk show kwenye Jiji la New York na hili vazi linaloonyesha mwili wake kwa asilimia kubwa kama unavyoona katika Picha hapo juu na Chini.Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa eonline.