Wednesday, June 12, 2013

HUYU NDO MWANAUME ANAESEMA PEPO ANAMTUMA KUMUUA MPENZI WAKE.


  Kijana wa miaka 26 Erick Onyango alimshangaza hakimu katika Mahakama ya Milimani Nairobi alipodai amepagawa na pepo anayemsukuma amuue mpenzi wake kwa kumchoma kisu.

 “Kuna pepo anayeniambia nimuue mpenzi wangu.Kwa kisu kisha nifungwe jela,” Bw Erick Onyango Onyango alidai kortini.

ERIC ONYANGO KATIKA PICHA.

Bw Onyango anayefanya biashara alikabiliwa na mashtaka 10 ya kumtumia Bi Lizzy Achieng Obonyo ujumbe wa vitisho na matusi.

Mshitakiwa huyo alishtakiwa kwamba mnamo Juni 9, 2013 alimtumia Bi Obonyo jumbe mfupi wa maneno wa vitisho katika simu yake ya mkononi.

Mnamo Juni 8 alimtumia mlalamikaji ujumbe mmoja. Mwezi uliopita wa Mei mwaka huu mshitakiwa alimtumia mlalamikaji ujumbe mwingine tena.

Bw Onyango alifikishwa mbele ya hakimu mkuu mwandamizi Bi Doreen Mulekyo.

No comments:

Post a Comment