Monday, June 24, 2013

IMERIPOTIWA TENA HALI YA MZEE MADELA KWA SASA SI NZURI KABISA.

Taarifa kutoka ikulu ya rais zilisema Jumapili jioni kuwa Mandela alikuwa amezidiwa ingawa madaktari wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa analejea kwenye hari yake ya kawaida.

Afisaa mmoja mkuu alisema kuwa raia wa Afrika Kusini wasiwe na matumaini kupita kiasi.

Mandela ambye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akiwa na umri wa miaka 94,alipelekwa hospitalini mapema mwezi huu, ikiwa ni mara ya tatu kwake kulazwa hospitalini akiugua ugonjwa wa mapafu mwaka huu.

Rais Jacob Zuma alisema Jumapili kuwa alimzuru Mandela Hospitalini na kuzungumza na mkewe kuhusu hali ya rais mstaafu.

Madaktari wanaomtibu Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.

Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.

Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.

Rais Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela na pia kuzungumza na jopo la matabibu wanaomtibu.

Baadaye bwana Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.

Na wakati huo huo leo majila ya saa 3 asubuhi kwa saa za Afrika kusini Rais Jacob Zuma atazungumza na waandishi wa habari(kwa saa za Afrika Mashariki itakuwa sa 4) na wachambuzi wa mambo wanasema mkutano huo ni kwa lengo la kuzungumzia ziara ya Rais wa marekani nchini Afrika kusini lakini pia swala la hali ya mzee Madela litachukua sehemu kubwa pia.

********************

KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI HABARI RAIS JACOB ZUMA KASEMA


“Former president Mandela remains in a critical condition in hospital. The doctors are doing everything possible to ensure his well being and comfort,” Zuma said.

Zuma reported that the 94-year-old’s health had deteriorated over the weekend, after he visited the icon’s bedside late Sunday.

“Given the hour that we got to the hospital it was late, he was already asleep,” Zuma said.

“(We) saw him and then we had a bit of discussion with the doctors and his wife Graca Machel.”

Zuma declined to give details about the health of his predecessor, who was rushed to hospital 17 days ago with a recurring lung infection.

“I don’t think I’m in a position to give further details, I am not a doctor. That is what I informed the country and the world and that remains the case for now,” Zuma said.


No comments:

Post a Comment