Saturday, June 15, 2013

MLIPUKO WATOKEA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA

WAKATI MWENYEKITI WA CHAMA AKIINGIA UWANJANI SOWETO

Kutoka mkoani Arusha Eneo la Soweto ni kwamba mda mfupi kuna mlipuko umetokea katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani uko Arusha kwenye mkutano wa Chama cha demokrasia Chadema katika eneo la Soweto na kuna majeruhi pamoja na vifo vya watu wawili katika tukio hilo...........!!!!Taarifa za awali toka mlipuko huo kutokea ni kuwa watu waliojeruhiwa katika mlipuko huo wanakimbizwa hospitali  tunaendelea kuwatafuta viongozi wa Chama walioko huko na pia wananchi walioko uko ila kada mmoja wa chama amesibitisha kutokea kwa tukio ilo mda mfupi uliopita,sasa tusubili taarifa rasmi kutoka kwa vyombo vya usalama pamoja na viongozi wa chama cha Chadema.Kama mwananchi na mpenda Amani kwa niaba ya blog hii tunawapa pole familia zilizopoteza ndugu na jamaa katika mlipuko huu na majeruhi wote tunawatakia nafuu na wapate matibabu kwa haraka zaidi. 

kama uko eneo lolote lile Arusha na unataka kutujulisha mambo yanaendeleaje katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha usisite kutufahamisha kupitia bpromas@outlook.com kwa wale wanaojua simu zetu tuendelee kuwasiliana pia.
live eneo la tukio SOWETO

1 comment:

  1. this is terrible situation ,the GOVT is supposed to investgate and calpture the culprits, the law be taken to place.

    ReplyDelete