Saturday, July 20, 2013

KWELI SERIKALI IMEFULIA KIFEDHA? PITIA RIPOTI HII...!!

Taarifa za ndani kutoka Wizara ya Fedha zinasema kwamba Serikali haina fedha kwa sasa ambapo sasa inalazimika kukusanya fedha kutoka katika mashirika yake ili kuendesha shughuli zake.

Miongoni mwa mashirika ya umma yanayoguswa na uamuzi huo wa Serikali ni mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwamo NSSF, PSPF, Mamlaka Udhibiti wa Nishati na Maji(Ewura)Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa(Tanapa), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na mengine kadhaa.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyakazi wa Idara za Fedha za mashirika hayo, walieleza kuwa kutokana uamuzi huo wa Serikali sasa wanalazimika kukaa ili kuandaa upya bajeti za mashirika hayo.

“Ukweli haya maagizo yana athiri kubwa kwetu kwani tayari tulikuwa tumepanga bajeti kutokana na mapato na kwa uamuzi huu ambao kimsingi hakuna mamlaka ya kuyapinga, itabidi tutoe, ila adhari zitakuwepo,”alisema ofisa mmoja wa juu wa moja ya mashirika ya umma.

Hata hivyo, alisema kuwa iwapo wangeshauriwa mapema basi walau wangetakiwa kuchangia asilimia tano kwa mwaka huu wa fedha na mwaka ujao ndipo ingeongezeka kufikia asilimia 10.

Ofisa mwingine wa shirika la umma aliyeomba kutotajwa jina alieleza kuwa uchangiaji huo, ulipaswa kutazama mashirika, kwani yapo yanayojiendesha kwa hasara, mengine yanapokea ruzuku na mengine yanajiendesha kwa fedha zake.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumamosi umebaini kwa Tanapa pekee inatakiwa kulipa Sh24 bilioni, zinazotakiwa kukatwa kutoka kwenye bajeti yao ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya shirika na jamii inayowazunguka.

Ukitaka kujua zaidi soma Ripoti hii ya Uchunguzi iliofanywa na Gazeti la Mwananchi.

 


No comments:

Post a Comment