Friday, July 26, 2013

MTOTO WA MWAKA MMOJA AKUTWA NA UJAUZITO.

  Mtoto wa mwaka mmoja nchini China ana ujauzito,Mtoto Kang Mengru wa nchini China alipelekwa hospitali baada ya wazazi wake kushtushwa na hali ya tumbo lake kuzidi kuwa kubwa siku hadi siku.

Baada ya mtoto huyo kufanyiwa ultrasound, madaktari waligundua kuwa mtoto huyo wa kike alikuwa

amebeba kitoto kichanga kwenye tumbo lake ambacho kilikuwa kikiendelea kukua.


Madaktari wanaamini kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa na mimba ya watoto wawili mapacha na pacha

mmoja alijitokeza ndani ya tumbo la pacha mwenzake.

Hali kama hiyo ya kichanga kuzaliwa ndani ya kichanga kingine ni nadra sana kutokea na humtokea

mwanamke mmoja katika wanawake 500,000.

Mtoto Kang atafanyiwa upasuaji kukiondoa kichanga hicho tumboni mwake.


No comments:

Post a Comment