Thursday, September 19, 2013

ALIYEHISIWA KUTOA USHAHIDI ICC KWA MARA YA KWANZA AIBUKA NA KUONYESHA WASIWASI WA USALAMA WAKE.

Picha hapo juu inamuonyesha mwanamke ambae  anahofia maisha yake baada ya kutambuliwa visivyo kwenye mitandao ya internet kwamba yeye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

Mwanamke huyo anasema aliathirika na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008 lakini yeye si shahidi katika makama ya ICC kama ilivyolipotiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mama huyo Rahab Muthoni Kagiri ,mwenye umri wa miaka 27 kutoka eneo la Burnt Forest , huko Rift valley anasema yeye sii shahidi katika kesi hiyo inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto pamoja na mtangazaji Joshua arap Sang.

Akionekana mwenye wasiwasi Bi Rahab asema sie yeye aliyesimama kizimbani kama shahidi wa kwanza katika kesi hiyo kinyume na inavyodaiwa na mitandao ya kijamii nchini Kenya.

Mama huyo anadia kuwa picha hiyo alipigwa na rafiki yake kwa lengo la kuiweka katika mtandao wake wa Facebook majira ya saa tano siku ya jumanne.

Lakini alishangaa saa mbili baadaye alianza kupigiwa simu na jamaa , ndugu na marafiki wakisema wameona picha yake katika mtandao ukisema yeye ndie shahidi aliyetoa ushahidi dhidi ya naibu Rais Wiliam Ruto.

Bi Rahab anasema japo yeye pia ni muathiriwa wa machafuko yaliotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1,00 waliuwawa lakini hajajitolea kutoa ushaidi katika mahakam hiyo ya ICC.

Na kutokana na madai ya ufichuzi wa mashahidi nchini Kenya , hii leo Mahakama ya ICC iliamuru shahidi wa kwanza ambaye alianza kutoa ushaidi wake siku ya jumatatu atoe ushahidi wake faraghani.

Hii nikutokana na kudaiwa kuwa na hofu nyingi

 Hii hapo juu ndio Picha iliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikisema huyo mwanamama ndio alikuwa shahidi wa kwanza kutoa ushaidi katika kesi hiyo na kupewa namba 536 na chini ni Mwanzo wa taarifa hizo zilipoanzia na kuanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.


No comments:

Post a Comment