Monday, September 23, 2013

HIZI NI PICHA NJISI WAZAZI WALIVYOKUWA WAKIJIFICHA KUOKOA MAISHA YA WATOTO WAO UKO KENYA,WATU ZAIDI YA 69 WAUWAWA.

Wakati hayo yakiendelea taarifa ni kwamba watu zaidi ya 69 wameuwawa kwenye sambulio hilo

Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini.

Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shuguuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuwanza kufyatua risasui kiholela.

Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya ya jengo hilo.

Helikopta za polisi zinapaa juu ya jengo hilo. Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.

Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaa waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.

No comments:

Post a Comment