Monday, September 23, 2013

ZAIDI YA WATU 60 WAUWAWA KENYA KWENYE SHAMBULIZI LA KIGAIDI LA AL SHAABAAB.

Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri wake wa usalama Joseph Ole Lenku imesema kuwa zaidi watu 59 wamefariki katika shambulizi la kigaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa.

Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi waliokua ndani ya jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano wakiwa wamjificha katika sehemu mbali mbali za jumba la Westgate.

Shirika la Red Cross awali katika taarifa yake ilisema kuwa watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara katika mashambulizi la kigaidi lililotokea Jumamosi mchana.

Milio ya risasi ilisikika katika jengo la Westgate mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawashikilia watu ndani ya jengo ilo ambao sasa ni mateka ambao idadi yao haijajulikana hadi sasa.

Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali wanazuiliwa ndani ya jengo hilo.

Watu 39 waliuwa baada ya wanamgambo hao kushambulia jengo hilo nje katika eneo la kuegeshea magari na badae kuweza kuingia ndani ya maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kuwpaiga watu risasi hovyo.

Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa. Rais Kenyatta anasema kuwa wale waliohusika lazima wakabiliwe na mkono wa sheria.

Jamaa na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa zao wamezuiwa kuingia ndani ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa walifariki kutokana na majeraha yao.

Picha hizi hapo chini ni njinsi mambo yalivyokuwa yakiendelea

 

 

No comments:

Post a Comment