Sunday, September 29, 2013

UPASUAJI WA KUKIONDOA KICHWA KILICHOJITOKEZA JUU YA KINGINE WAFANIKIWA.

Picha hii inamuonyesha Mtoto ASREE GUL wa miezi mitatu aliezaliwa na kichwa cha ziada kama kinavyoonekana katika picha akiwa Hospitalini.Mama wa Asree Gul alijifungua mapacha wa kike mmoja alikuwa na afya nzuri ila mwingine ambae ndie Asree alibainika kuwa na matatizo ya kichwa kama anavyoonekana katika picha.Asree alikuwa anapata shida sana kwenye kulala vizuri na pia alikuwa ananyanyapaliwa sana kijijini kwao ili kuokoa maisha yake wazazi wake waliamua kwenda kuwaona Madaktari ili kuweza kukiondoa kichwa kilichoota juu ya chezake na hatimaye Operation ilifanyika kwa umakini sana na Mungu akamjalia ikafanikiwa na kukiondoa kichwa hicho kilichokuwa kimejisikiza kwenye kichwa kingine.Madaktari wanasema aikuwa kazi rahisi kuifanya operation hiyo maana ilibidi kukabiliana na mishipa muhimu kama ya Damu na ugumu wa fuvu la pili.

Picha ya chini  ni baada ya upasuaji Mtoto ASREE GUL akiwa na Pacha mwezake kulia kwake.

 


No comments:

Post a Comment