Tuesday, October 1, 2013

ALIETUHUMIWA KUMTEKA DR,ULIMBOKA ALIPA FAINI YA SH 1000 HII NDO SHERIA INAVYOSEMA KWA KOSA KAMA HILO.

Joshua Mulundi (21) raia wa Kenya aliyekuwa anatuhumiwa kumteka na kumtesa Dk Ulimboka na baadaye kuachiwa huru na mahakama na baadaye kufunguliwa kesi ya kulidanganya jeshi la polisi, ahukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela ama kulipa faini ya shilingi elfu moja (1000) baada ya kukili kosa lake.

Hata hivyo mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa faini hiyo na hivyo kuachiwa huru.Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu mkazi Aloyce Katemana baada ya wakili wa serikali kusoma maelezo ya mshitakiwa kwamba alikili kutoa taarifa za uongo kwa jeshi la polisi.Kabla ya hukumu hiyo kutolewa mshitakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ilo ni kosa lake la kwanza kulifanya.
Pia alijitetea kuwa Juni 27, 2012 akiwa Arusha alitekwa na kupelekwa Dar es Salaam ambako alikuwa hana mwenyeji wala hakuwahi kufika.

Alisema kutokana na kutekwa huko alichanginyikiwa hivyo kukubali chochote alichoambiwa afanye kwa kuwa aliyemteka alikuwa na silaha na alimwelekeza mambo ya kuzungumza.

“Mheshimiwa kwa ajili ya vitisho hivyo, nilikwenda Kawe katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko kwenye eneo la Tanganyika Packers, mbele ya Mchungaji Joseph Malwa Kiliba na kuungama kuwa ni miongoni mwa watu waliomtesa Dk Ulimboka katika Msitu wa Pande,” alisema Mulundi na kuongeza:

“Siwalaumu Serikali, upande wa mashtaka wala polisi kwa kitendo cha kuniweka gerezani kwa muda mrefu, najilaumu mimi mwenyewe.”

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Kweka aliiambia Mahakama kuwa hana kumbukumbu za uhalifu za mshtakiwa lakini aliomba apewe adhabu kali kutokana na mazingira ya tukio hilo.

Akitoa hukumu, Hakimu Katema alisema alifikia uamuzi huo kwa kuzingatia maombi ya mshtakiwa ya kupunguziwa adhabu.


No comments:

Post a Comment