Tuesday, November 5, 2013

ANAISHI KWENYE KABURI NA MIFUPA YA RAFIKI YAKE KWA MIAKA 13.

Fabio Beraldo raia wa Blazil anaishi kwenye kaburi la rafiki yake kwa miaka 13 sasa na zaidi sana analala sambamba na mabaki ya mwili wa rafiki yake kama anavyoonekana katika Picha hapo juu.Alipoulizwa kwa nini analala kwenye kaburi alisema "Mimi ninahofu ya maisha lakini sina hofu ya kuwa na wafu maana nikiwa hapa nakuwa na Amani na ni sehemu tulivu kwangu.Akielezea hadi kuanza kuishi hapo alisema siku mmoja alipokuwa akitembea usiku huku akiwa ameisha jiusisha na maswala ya uvutaji bangi mvua ilinyesha sana na ilipoisha na kupapazuka alijikuta yuko huko lakini akumbuki alifikaje makaburini na hapo ndipo alipoanza kuishi huko kwa miaka 13 sasa.Maisha yake kwa sasa analala Makaburini na Asubuhi anapita katika mitaani kuomba chochote kitu.

KWELI DUNIANI KUNA MAMBO.

********************

No comments:

Post a Comment