Thursday, February 13, 2014

FIFA YATOA RUKSA OKWI KUCHEZA YANGA.

Habari zilizotufikia mchana huu ni kwamba Shilikisho la kandanda Ulimwenguni Fifa limefikia maamuzi ya kumruhusu mshambuliaji wa Zamani wa Simba na Etoile Du Sahel ya Tunisia na badae Villa ya Uganda Emmanuel Okwi kuichezea timu hiyo ya mitaa ya Twinga na Jangwani ya Jijini Dar es salaam Tanzania.

Okwi ambaye alikuwa amesimamishwa kutokana suala la mgogoro mauzo yake uliokuwa ukizihusisha timu zake za zamani Simba SC ya Tanzania na Etoile Du Sahel ya Tunisia, sasa ameruhusiwa kuitumikia Yanga huku FIFA ikiendelea kufuatilia kiundani kuhusu deni la Simba la dola 300,000 wanaloidai Etoile.


No comments:

Post a Comment