Monday, April 14, 2014

HATIMAYE HATI HALISI YA MUUNGANO ITAWASILISHWA BUNGENI SIKU MBILI ZIJAZO.

Mwenyekiti wa kamati namba Sita Mh.Stephen Wasira kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amethibisha rasmi leo ndani ya Bunge la Katiba na kwa wananchi wa Tanzania kuwa Hati alisi ya Muungano ilisainiwa na Marais wawili Mwl.Julius Nyerere na Mwezake Abed Karume miaka hamsini iliopita ipo na itwasilishwa rasmi katika Bunge la Katiba ndani ya siku mbili zijazo,namnukuu Wassira: Nalihakikishia Bunge kuwa Hati ya Muungano wa Tanzania ipo na itawasilishwa Bungeni siku mbili zijazo!

Kwa hatua hiyo ya kuitoa Hati halisi ya Muungano itakuwa imesaidia kupunguza maneno kutoka Baadhi ya wajumbe kuwa hati hiyo aipo na kama ipo basi si halisi bali itakuwa imechakachuliwa.

Wakati mijadala ya kamati ikiwa inaendelea kuliibuka swala la wajumbe kutaka wapatiwe hati ya muungano na hata ilipopatikana ilionekana kama baadhi ya saini zilizopo zimegushiwa.

 Leo aliekuwa Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya muungano mzee Pius Msekwa alipokuwa amazungumza kupitia kituo cha tv cha Taifa (TBC1) Amesema kuwa kuwa hakuwahi kuziona na wala hazikuwahi kuletwa bungeni badala yake, kile kilicholetwa bungeni ile tarehe 25/04/1964, ili kuridhia hati hizo, sio Hati Halisi za Muungano, bali ililetwa Sheria ya Muungano, ikiwa imeambatanishwa na "a schedule" ya Hati Hizo, iliyokuwa imepigwa chapa tuu, bila saini yoyote!.

 


No comments:

Post a Comment