Friday, March 21, 2014

ANA MIEZI 8 KILO ZAIDI YA 20.

Santiago Mendoza mtoto mwenye umri wa miezi 8 sasa anasadikika ndio mtoto mnene zaidi akiwa na uzito wa kilo 20 sawa na mtoto wa miaka 6 huko nchini Colombia!

Mama yake anakiri kuwa uzembe wake ndio uliosababisha mtoto wake awe na uzito mkubwa kuliko kawaida kwani kila mtoto huyo anapolia amekuwa akimshindilia misosi na maziwa ili anyamaze kitu kilichopelekea uzito kuongezeka kwa kasi!

Kwa sasa mtoto huyo amepewa msaada wa kupelekwa  sehemu wanayoweza kuokoa maisha yake kwani amekuwa akilazwa kila mara kutokana na  uzito wake kuwa mkubwa kitu kinachoweza kuleta madhara makubwa kiafya... kilo 20 miezi 8 si kawaida.

 


No comments:

Post a Comment