Tuesday, June 11, 2013

HIZI NDIZO SABABU NNE ZINAZOFANYA OBAMA KUJA TANZANIA YASEMA MAREKANI.

 Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt alisema sababu ya kwanza ya Obama kuja Tanzania ni kutokana na kuwa mfano wa utawala bora, demokrasia na ushirikishaji wa watu wake wakati wa kufanya uamuzi unaogusa maisha yao ya kila siku.

Alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano linapokuja suala la uongozi bora na ndiyo maana imekuwa na amani na utulivu kwa muda mrefu ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Nchi nyingi za Afrika zinazoizunguka Tanzania zimekuwa na matatizo ya vita vya wenyewe na hata ukosefu wa utawala bora,” alisema Balozi Lenhardt ingawa alidokeza kuwa katika siku za karibuni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani.

Balozi Lenhardt alisema sababu nyingine inayomfanya Rais Obama kuja Tanzania ni kutokana na jitihada za Serikali ya Marekani kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kasi ya ukuaji wa uchumi.

“Rais Obama anakuja kuunga mkono juhudi za Watanzania katika kutengeneza mazuri ya uwekezaji lakini bila kusahau kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania imeivutia Serikali ya Marekani,” alisema.

Balozi Lenhardt alitaja sababu nyingine inayomleta Rais Obama kuwa ni kuisaidia Tanzania kuendeleza fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo.

Alisema uendelezaji huo wa fursa una lengo la kuisaidia Serikali ya Tanzania kukabiliana na tatizo la umaskini.

Alisema Marekani ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kutoa fedha nyingi za misaada na akisema kwa mfano, mwaka 2012 pekee ilitoa Dola 750 milioni.

Aidha, alisema nchi yake imekuwa ikitoa misaada mingi kupitia Shirika la Millenium Challenge (MCC), ambayo imejikita zaidi katika kusaidia sekta za umeme, maji na miundombinu.

Rais Obama atakuwa ni rais wa tatu wa Marekani kuja kuitembelea Tanzania watangulizi wake waliomtangulia ni pamoja na Bill Clinton na George Bush.

  ******************************************************

 

US ambassadar Alfonso Lenhardt said Mr Obama chose to visit Tanzania and not other countries in the region because it is a beacon of peace on the continent, an important investment destination and a global champion in the fight against poverty.

“The visit by President Obama is precisely to support Tanzania in its development endeavours and to deepen the bilateral cooperation between the great countries,” Mr Lenhardt said.

He said the US was supportive of China’s relations with Tanzania if the purpose was legitimate and the focus was the country’s development. “We are supportive of China’s relations with Tanzania provided the purpose is legitimate. China does not pose a problem one way or the other, but the issue should be how we help Tanzania become a medium income country.”

Tanzania will be the last stop of Mr Obama’s three-nation tour of Africa from June 26 to July 1. President Obama, who will also visit Senegal and South Africa, will be accompanied by his wife Michelle and daughters Malia and Sasha.

Mr Lenhardt said the itinerary and exact agenda of Mr Obama’s visit was not yet unclear, but added that he would meet stakeholders from the private and public sectors as well as youth representatives.

“We do not yet know exactly which specific agenda the President has in those focus areas, but the general purpose of the visit is to reinforce the bilateral cooperation between the two countries.”

Taking stock of US-funded aid programmes in Tanzania, the ambassador noted that his government supported projects worth about $750 million (Sh 1.2 trillion) million last year, making it one of the country’s biggest development partners. He said through the United States Agency for International Development (USAID) and other nine agencies, the US had invested in various sectors that touched on the wellbeing of the majority Tanzanians by improving their health, food security and democracy and leadership.

Mr Lenhardt said the funds given were a sign of American people wanting to reach out to Tanzanians and improve their lives, adding that there was no hidden agenda.

No comments:

Post a Comment